Waliotoa maoni yao siku hiyo ni kutoka: Jumuiya ya Wanahabari ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Global Online TV, Ayo TV na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Wanaotakiwa kujitokeza kutoa maoni kesho Ijumaa Novemba 3, 2023 ni: Taasisi za ndani za vyombo vya habari na wasimamizi wa sekta: Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Kalabu za Habari za Mikoa Tanzania (UTPC), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),MISA-TAN, TMF na KADIO.
Aidha, kamati imeanza awamu ya pili ya kusambaza madodoso juu ya suala hilo yanayotakiwa kujazwa na waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi walio kwenye vyombo vya habari.
Kamati iliyopewa jukumu hilo ina wajumbe wafuatao: Tido Mhando (Mwenyekiti), Dkt. Rose Reuben (Makamu Mwenyekiti), Mobhare Matinyi (Katibu), Sebastian Maganga, Richard Mwaikenda, Bakar Machumu, Joyce Mhavile, Kenneth Simbaya na Jacqueline Woiso.
Post a Comment