Featured

    Featured Posts

WCF YATEKELEZA KWA KISHINDO ILANI YA CCM, IMELIPA FIDIA SH. BILIONI 65.4 HADI KUFIKIA SEPTEMBA 2023, NI ENDELEVU KULIPA FIDIA HADI 2047/48

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mainduzi (CCM) ya 2020-25, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeonekana kufanikiwa kwa kishindo, tangu ulipoanza rasmi Julai Mosi, 2015, na kupewa mwaka mmoja (grace period) kabla ya kuanza rasmi ulipaji wa mafao ya fidia kwa walengwa.

Hali ya Mfuko huo kuonekana kufanikiwa, japokuwa inawezekana ni ya muda mrefu, binafsi nimeibaini leo Novemba 2, 2023, katika Mkutano baina ya Uongozi wa WCF na Wahariri wa Habari, ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika katika Ukumbi wa Victoria House, Jijini Dar es Salaam.

Akieleza katika mkutano huo, Utendaji na mafanikio, Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dk. John Mduma, alisema hadi kufikia Septemba mwaka huu (2023) Mfuko huo umeshalipa fidia kiasi cha sh. Bilioni 65.4, Mfuko ukiwa umeweza kusajili asilimia 95 ya waajiri wote wanaostahili na kuahidi kuwa Mfuko uko mbioni kukamilisha asilimia 5 ya waajiri ambao bado hawajajisajili.

Dk. Mduma alinadi pia kwamba, hadi sasa Mfuko una uwezo endelevu wa kulipa fidia hadi mwaka wa fedha 2047/2048, akisema hiyo ni kwa mujibu wa tathmini ya uhai na uendelevu wa Mfuko ya mwaka 2018, iliyofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), sanjari na tathmini ya pili iliyofaywa ya WCF yenyewei mwaka 2022 iliyoonyesha kuwa Mfuko ni himilivu na una uwezo wa kuendelea kutoa huduma bila kutetereka.

Alisema katika utendaji wake, WCF sio tu inalinda nguvu kazi ya taifa, pia inajivunia kuwamba waajiri sasa wana muda mrefu wa kuendelea na kazi za uzalishaji huku jukumu la kumhudumia mfanyakazi aliyeumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi nalo likibebwa na Mfuko huo.

“Lakini pia uwepo wa WCF umeleta tija kazini kutokana na mahusiano mazuri kati ya waajiri na waajiriwa, na pia kupunguza umaskini hususan kwa wategemezi na wafanyakazi wanaopata ulemavu wa kudumu na kushindwa kurudi kazini au kufariki.” Alisema.

Alisema Mfuko unachangia ongezeko la uzalishaji na maendeleo ya Taifa kupitia ongezeko la tija, ongezeko la pato la taifa na kodi ili kuiwezesha Serikali kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi

Akiendelea kueleza mafanikio, Dk. Mduma alisema pia kwamba, kutokana na mafanikio ambayo Mfuko umeyapata, umekuwa kinara na umeweza kuwafanya majirani toka nchi za Zambia, Kenya, Botswana, Afrika Kusini na Zimbabwe kujifunza kutoka WCF.

Kuhusu majukumu ya WCF, Dk. Mduma alisema, ni pamoja na Kusajili Waajiri waliopo katika Sekta ya Umma na Binafsi Tanzania Bara, Kukusanya michango kutoka kwa Waajiri, Kulipa Fidia kwa Mfanyakazi anayeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.

Majukumu mengine alitaja kuwa ni kutunza kumbukumbu za matukio ya ajali, magonjwa na vifo kutokana na kazi, kukuza mbinu za kuzuia ajali, magojwa na vifo kutokana na kazi na kuelimisha umma kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) yenye jukumu la kusimamia utendaji wa Mashirika yote ya Umma nchini ,Thobias Makoba, alisema Ofisi hiyo imeweka utaratibu kwa viongozi wa taasisi hizo kukutana na wahariri wa habari ili kuueleza umma hali halisi ya utendaji wao na hadi hadi sasa taasisi kadhaa zimeshafanya hivyo.

“Kwa mantiki hiyo Ofisi ya Msajili wa Hazina ikaona umuhimu na msingi wa kuzikutanisha taasisi za umma na umma wenyewe kupitia Wahariri hawa habari, ili wapate kwenda kuujulisha umma utendaji wao na lengo sio tu kutoa elimu, lakini iwe ufunguo kwa taasisi kufanya muendelezo wa kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari", akasema Makoba.

Akifafanua zaidi alisema Msajili wa hazina anaelekeza mara kadhaa kwa taasisi za umma kila zinapoandaa taarifa za fedha za kila mwaka wahakikishe zinatangazwa ili umma ujue mwenendo wa mashirika yao. "Umma ukiwa na uelewa wa kutosha itakuwa rahisi kwao kubaini usahihi wa kinachoelezwa kuhusu taasisi fulani." akasema Makoba.

Akitoa neno la shukurani, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, alisema utaratibu uliobuniwa na Ofisi ya Msajili wa hazina wa Wakuu wa taasisi kukutana na Wahariri na kutoa taarifa za kina kuhusu utendaji limejenga nafasi nzuri ya kuufanya umma na hata wahariri wenyewe kujua mengi ya taasisi na kuishukuru Ofisi hiyo ya Msajiliwa Hazina kwa ubunifu huo.

“Lakini hapa nataka niwaambie ninyi wahariri na hawa ndugu zetu wanaofaidika na fidia, muwe mabalozi wa Mfuko huko muendako ili Watanzania wengi zaidi waweze kufaidika na huduma za WCF.” alisema Balile.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi (WCF) Dk. John Mduma, akitoa wasilisho katika kikao kazi na Wahariri wa Habari, kuelezea utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya WCF, miaka 8 tangu kuanzishwa kwake jijini Dar es Salaam, leo Novemba 2, 2023. Wengine ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusaino Ofisi ya Msajili wa Hazina Thobias Makoba.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusaino Ofisi ya Msajili wa Hazina Thobias Makoba akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyeiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini, WCF Dk. Adulsalaam Omar akizungumza katika mkutano huo.
Anselim Peter, Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF.
Baadhi ya Washiriki.
Baadhi ya washiriki.

WASILISHO LILILOTOLEWA NA DK. MDUMA KATIKA MKUTANO HUO HILI HAPA 👇
Wasilisho hilo, lilikuwa lina annecure mbili (2) za nyongeza kutoka kwa DO na DAS.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana