Na CCM Blog
Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauari Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Philip Mpango amezungumza na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, baada ya kurejea nchini alikokuwa na majukumu maalum aliyotumwa na Rais.
Akizungumza katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, amemweleza Rais Dk. Samia kwamba pamoja na aliyozushiwa yote katika baadhi ya mitandao ya kijamii amerejea akiwa mzima mweneye afya njema.
Mbele ya Rais, Dk. Mpango ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Watanzania wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya, kwa kuwa kufanya tabia hiyo husababisha taharuki na huzuni kwa ndugu, jamaa, marafiki na kwa watumishi wanaofanya kazi na anayezushiwa taarifa za uongo.
Akitoa mfano wa namna taarifa za uongo zinavyoumiza familia za wanaozushiwa, alisema mwaka 2021 alipozushiwa kifo Dada yake aliyekuwa na umri wa miaka 80 ambaye kwa sasa ameshafariki alianguka kutokana mshtuko.
"Mhe. Rais nina afya njema tayari kuendelea na kazi ukiacha hizo maalum ambazo nilikuwa nashughulika nazo (Nje ya Nchi), nawashukuru sana Viongozi wote na Watanzania ambao baada ya kupata taarifa ambazo hazikuwa sahihi walipata taharuki kubwa, wengi wameniombea sana ninawashukuru kwa moyo wangu wote na hao wachache ambao wanasema maneno mengine basi nawaombea msamaha kwa Mungu.
Natumia nafasi hii kuwaomba Watanzania wenzangu mitandao ni chombo kizuri lakini matumizi yake nawaomba tutumie mitandao vizuri, unajua ukisema huyu Mzee amekata moto wengine wanaweka picha yangu na mshumaa unawaka lakini Mh. Rais sisi viongozi ni binadamu tuna watoto tuna wajukuu, tuna familia ,tuna marafiki na Wafanyakazi wenzetu, wanakumbwa na taharuki kubwa sana ambayo haina sababu," akasema Dk. Mpango na kuongeza;
"Mwaka 2021 Dada yangu ambaye nilimzika mwezi wa nane, alipoambiwa kwamba Mimi Mwanae kwasababu alinilea nimefariki alianguka akiwa Mama wa miaka 80, sio mambo mema ni vizuri tutumie mitandao kwa mema kuwatakia kheri Watanzania wenzetu", akasema Dk. Mpango na kuongeza;
Mhe. Rais uliponiapisha nilisema unitume mchana na usiku, ulinituma huko Nje ya Nchi, nimerejea nchini tayari Kuendelea na kazi, nikiwa na afya njema”.
Tafadhali msikilize hapo👇
Post a Comment