Featured

    Featured Posts

SADIO MANE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA


NYOTA wa Senegal, Sadio Mane ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika kufuatia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool na kuifikisha timu yake ya taifa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.Mane mwenye umri wa miaka 27, ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushika nafasi ya pili mbele ya mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah wa Misri miaka ya 2017 na 2018 na kushika nafasi ya tatu mwaka 2016. Anakuwa mchezaji pekee kutoka Senegal kushinda tuzo hiyo baada ya El Hadji Diouf, aliyeshinda mara mbili, mwaka 2001 na 2002.

Winga wa Senegal, Sadio Mane ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika 

WASHINDI WOTE WA TUZO ZA CAF 2020 

Mchezaji Bora wa Kiume wa Mwaka: Sadio Mane
Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka: Asisat Oshoala
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka: Achraf Hakimi
Timu ya Mwaka: Onana, Aurier, Matip, Koulibaly, Hakimi, Gueye, Mahrez, Zyech, Salah, Aubameyang, Mane
Goli Bora la Mwaka: Mahrez (mpira wa adhabu Nusu Fainali AFCON)
Kocha Bora wa Mwaka: Djamel Belmadi
Kocha Bora wa Kike wa Mwaka: Diseree Ellis
Timu Bora ya Mwaka: Algeria
Timu Bora ya Mwaka ya Wanawake: Cameroon
Mane ameshinda tuzo hiyo baada ya kura zilizopigwa na makocha wakuu, Wakurugenzi wa Ufundi na Manahodha wa timu za taifa za wakubwa kutoka nchi wanachama wa CAF.
Naye Achraf Hakimi anayecheza kwa mkopo Borussia Dortmund kutoka Real Madrid alishinda tuzo ya Mwanasoka Chipukizi.
Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka imechukuliwa na  Djamel Belmadi baada ya kuiwezesha Algeria kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.
Nyota wa Ligi Kuu ya England, Serge Aurier wa Totenham, Joel Matip wa Liverpool, kiungo wa zamani wa Everton, Idrissa Gueue, nyota wa Manchester City, Riyad Mahrez na Nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang wamejumuishwa kwenye Timu ya Mwaka pamoja na Mane na Salah.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana