Rais wa Malawi Dk. Lazarus Chakwera tayari amekwishawasili nchini, ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Hii ni ziara rasmi ya Kitaifa ya kwanza kwa Mhe. Rais Dkt. Chakwera tangu aingie madarakani mwezi Juni, 2020 yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na kuendelea kudumisha ujirani mwema.
Rais Chakwera atatembelea Bandari ya Dar es Salaam ili kujionea shughuli mbalimbali za bandari hiyo na uboreshaji wa miundombinu ya bandari ambayo itaharakisha utoaji wa mizigo bandarini na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora bandarini hapo lakini pia atatembelea kituo cha kuhifadhia mizigo cha Malawi ambacho kimekuwa alama muhimu ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi.
Rais. Dkt. Chakwera akiwa na mwenyeji wake, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, wataweka jiwe la msingi katika Kituo cha Mabasi ya kwenda mkoani cha Mbezi Mwisho.
Uhusiano kati ya Tanzania na Malawi ni mzuri na unaendelea kuimarika siku hadi siku.
Post a Comment