Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi watatu walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho, Ikulu jijini Dar es Salaam ni David William Cancar (aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Uingereza hapa nchini), Muhammad Saleem (aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Pakistan hapa nchini) na Didier Chassot (aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Uswisi hapa nchini).
Balozi wa Uingereza hapa nchini, David William Cancar amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake mzuri ambapo Tanzania kwa kufanikiwa kuingia katika uchumi wa nchi za kipato cha kati, kusambaza umeme kwa kasi kubwa, kutoa elimu bure, kujenga miundombinu hasa barabara.
“Tumekuwa na mazungumzo mazuri na Rais Magufuli, tunatazamia kukuza zaidi uhusiano wa Uingereza na Tanzania hasa katika biashara, kwa sasa biashara yetu ni takribani Bilioni 390 kwa mwaka na pia tunachangia takribani Bilioni 800 kwa mwaka katika miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Tanzania. Matarajio yangu ni kuwa tutaongeza Zaidi,” David William Cancar
TAZAMA BALOZI AVUA BARAKOA MBELE RAIS MAGUFULI, AMPONGEZA JPM IKULU
Post a Comment