Mbunge wa zamani wa Kilwa Murtaza Mangungu akizungumza baada ya kushinda Uenyekiti wa Simba katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika leo katika Ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam, leo.
JNCC, Dar es Salaam
Mbunge wa zamani wa Kilwa Murtaza Mangungu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Simba katika Uchaguzi mdogo uliofanywa na Wanachama wa Klabu hiyo katika Ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam, leo.
Murtaza amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo baada ya kumsinda aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa zamani wa jimbo la Chemba Juma Nkamia kwa kura 472, baada ya kupata kura 802, huku Nkamia akiambulia kura 330.
Post a Comment