Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Wanachama wa Klabu ya Simba leo wanafanya Uchaguzi mdogo wa kumpata Mwenyekiti wa Klabu hiyo, katika Ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam, mchuano ukiwa ni kati ya wagombea wawili tu ambao ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa zamani wa jimbo la Chemba Juma Nkamia na Mbunge wa zamani wa Kilwa Murtaza Mangungu.
Katika Uchaguzi huo, Nkamia ambaye amewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Simba anatazamiwa zaidi kuitwaa nafasi hiyo kuliko Mangungu na Nkamia na Mangungu walipitihwa hivi karibu katika mchakato uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti wake Boniface Lihamwike.
Uchaguzi huo unafanyika kukiwa hakuna mshikemshike mkubwa wa wagombea wengi, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya waliokuwa wameomba kugombea kujitoa.
Wadadisi wa masuala ya soka nchini wanadai kwamba msikemshike umekuwa hakuna kutokana na nafasi ya Mwenyekiti kwenye Klabu hiyo kuwa kama ya kukamilisha safu tu kwa kuwa Mwenyekiti kwenye Klabu hiyo hana nguvu ya kusimamia au kutoa maamuzi.
Inaelezwa kwamba Mwenyekiti hana maamuzi kwa kuwa kulingana na Katiba ya Klabu hiyo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye kwa sasa ni Mohammed Dewji, na Bodi hiyo ndiyo yenye maamuzi ya mwisho ya hatma ya Klabu.
Hali hiyo ya mwongozo wa Katiba inamfanya Mwenyekiti asiwe na maamuzi makubwa kwa kuwa anashiriki kwenye Vikao vya Bodi kama mjumbe miongoni mwa wajumbe wengine.
Baadhi ya wanachama waliofika ukumbini wakisajiliwa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo.
Post a Comment