Featured

    Featured Posts

RAIS AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 12 Septemba, 2021 amefanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi kama ifuatavyo:-


Amemteua Mhe. Dkt. STERGOMENA LAWRENCE TAX (Mb), kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.  Mhe. Dkt. TAX anachukua nafasi ya Marehemu ELIAS JOHN KWANDIKWA. 


Amemteua Dkt. ASHATU KACHWAMBA KIJAJI (Mb), kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.  Mhe. Dkt. KIJAJI anachukua nafasi ya Dkt. FAUSTINE E. NDUGULILE (Mb), ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Aidha, Mheshimiwa Rais ameihamishia  Idara ya Habari katika Wizara hii kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.   


Amemteua Mhe. JANUARY YUSUF MAKAMBA (Mb), kuwa Waziri wa Nishati.  Mhe. MAKAMBA anachukua nafasi ya Dkt. MERDARD MATOGOLO KALEMANI (Mb), ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


Amemteua Mhe. Prof. MAKAME MNYAA MBARAWA (Mb), kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.  Mhe. Prof. MBARAWA anachukua nafasi ya Mhandisi Dkt. LEONARD MADARAKA CHAMURIHO (Mb), ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


Amemteua Dkt. ELIEZER MBUKI FELESHI, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. FELESHI alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. 


Mawaziri Wateule pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wataapishwa tarehe 13 Septemba, 2021 saa 05:00 asubuhi, Ikulu - Chamwino, Dodoma.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana