Featured

    Featured Posts

TAARIFA YA MAFANIKIO YA MKURABITA KATIKA MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

 UTANGULIZI

 Katika utekelezaji wa urasimishaji nchini, MKURABITA inaendelea kutumia mfumo wa kuzijengea uwezo wa urasimishaji Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara sambamba na kujenga uwezo wa Wizara za Kisekta kwa upande wa Zanzibar ambazo ni Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi; na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda. 

Katika kipindi cha mwaka mmoja wa serikali ya Awamu ya Sita utekelezaji wa shughuli za MKURABITA umezingatia mambo makuu yafuatayo:- 

 i. Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020;

 ii. Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III);

 iii. Hotuba ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa wakati wa kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

 iv. Hotuba ya Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyoitoa wakati wa kuzindua Baraza la Tisa (9) la Wawakilishi;

 v. Hotuba ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa wakati wa kuapisha Makatibu wakuu; 

 vi. Maagizo mbalimbali ya Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na 

 vii. Maagizo ya Kamati ya |Uongozi ya MKURABITA. 


 2. MAFAMIKIO YA UTEKELEZAJI MACHI 2021 HADI MACHI 2022 

 Katika kipindi cha utekelezaji cha kuanzia Machi, 2021 hadi Machi, 2022 Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha MKURABITA kutekeleza majukumu yake na kupata mafanikio makubwa ya kuwawezesha wananchi kiuchumi. Muhtasari wa Mafanikio yaliyopatikana ni kama ifuatavyo: 

- 2 i. MKURABITA imepokea jumla ya shilingi Milioni 978.0 kutoka Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ya ujenzi wa masjala za vijiji 22 katika halmashauri 14 za Tanzania Bara. MKURABITA katika kutekeleza lengo la ujenzi wa masjala na kusogeza huduma karibu na wananchi ilihakikisha uwepo wa thamani ya fedha inayotumika (Value for Money) kupitia mwongozo wake wa utekelezaji kwakusaini Randama ya Makubalianao (MOU) na Halmashauri zote husika na kutuma fedha za ujenzi katika akaunti za vijiji vyote husika ambapo ilisimamia utekelezaji wake kwa kushirikiana na Halmashauri hizo. 

Masjala zilizokamilika kwa asilimia 100 mpaka sasa ni pamoja na vijiji vya; Mabadaga (Mbarali), Sambarai na Kindi (Moshi), Maweni na Karangai (Meru), Manyemba (Chamwino), Lupaso na Mpeta (Masasi), Chilangara na Mitema (Newala), Nakalonji (Nachingwea), Inzomvu (Mpwapwa) na Gurungu (Itigi). Aidha masjala za Jaribu Mpakani (Kibiti), Melela (Mvomero), Nahimba (Nachingwea), Mshani (Sumbawanga), Mwakauta (Makete), Kileo, Kirya na Lembeni (Mwanga) na Katuka (Kalambo) zimekamilika kwa asilimia 98 kutokana na changamoto ya kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi. Masjala ya Malembuli (Makete) ujenzi wake ulianza Januari 2022 na sasa umefikia 15% wakati masijala za vijiji vya Membe (Chamwino), Makanda na Msisi (Bahi), Naming’ong’o (Momba) na Lukani (Kilolo) zinafanyiwa upembuzi yakinifu ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Machi 2022. 

Kwa Upande wa Zanzibar upembuzi yakinifu utafanyika mwezi wa Machi 2022 ili kuwezesha ujenzi wa ofisi ya Sheha katika Shehia ya Makunduchi kuanza mwezi April 2022. 

 ii. Kwa kushirikiana na taasisi za fedha, Maafisa Ugani, Maafisa Maendeleo, Maafisa Mifugo na Maafisa Ushirika wa Halmashauri, MKURABITA imetoa mafunzo kwa wamiliki 2,400 wa mashamba yaliyorasimishwa juu ya matumizi hati miliki za kimila kiuchumi na kufanya kilimo biashara katika halmashauri za Wilaya za Mufindi (395), Kilolo (220), Sikonge (507), Butiama (210), Moshi (706), Rufiji (147) na Kibiti (215).

 Aidha, jumla ya mizinga 30 ya nyuki imetolewa kwa wananchi wa Kijiji cha Lugodalutali wilaya ya Mufindi. Kwa namna ya kipekee, MKURABITA imejenga uwezo wa matumizi ya ardhi kiuchumi kwa kutoa 3 mafunzo kwa wananchi (58), wa jamii ya kifugaji ya kimasai ambao mashamba yao yamerasimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali;

 iii. MKURABITA imepima jumla ya mashamba 562 na jumla ya Hati za Haki Milki za Kimila 487 zimeandaliwa na kutolewa katika Halmashauri za wialaya za Chamwino (106), Kilosa (161) na Kilolo (220).

 Aidha, kazi ya kupima mashamba 1,084 ya mazao ya chai na parachichi katika vijiji nane (8) wilayani Kilolo inaendelea na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi machi. iv. MKURABITA imekamilisha upimaji wa mashamba na viwanja 3,649 ya wakulima wa Miwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambapo mashamba na viwanja 1,610 yamepimwa na kuidhinishwa. 

Jumla ya Hati 758 zimeandaliwa na kusajiliwa. Kazi ya Kukamilisha uandaaji wa hati miliki zilizobaki inaendelea na inatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Juni 2022. Aidha, kazi ya kukamilisha uandaaji wa Hati Miliki 2,818 katika Halmashauri za wilaya ya Makete (1,200), miji ya Tunduma (1,118) na Babati (500) inaendelea na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa April 2022. 

 v. Kwa upande wa Zanzibar, MKURABITA imeshirikiana na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, na hivyo kuwezesha kupima jumla ya viwanja 2,800 na kuandaa hati 248 za matumizi ya ardhi. 

Aidha, jumla ya hati 89 zimetolewa kwa wananchi wa Shehia ya Welezo; 

Wizara inaendelea na utambuzi wa viwanja 9,404 katika maeneo ya Jambiani, Meya, Mahonda, Kidoto, Fuoni, Mombasa na Kwa Mchina. vi. Utafiti wa msingi (Baseline survey) umefanyika kwa wafanyabiashara 11,956 katika Halmashauri za Majiji ya Mbeya (1,353), Ilala (1,562), Dodoma (2,077), Manispaa za Musoma (1,231), Iringa (1,222), Moshi (2,173) na Shinyanga (2,338). Kati yao jumla ya wafanyabiashara 7,850 wamepata mafunzo ya namna bora ya kuendesha biashara endelevu na shindani katika majiji ya Mbeya (825), Ilala (889), Dodoma (1,360), Manispaa za Musoma (700), Iringa (680), 4 Moshi (1,696) na Shinyanga (1,700). 

Kwa upande wa Zanzibar, Wafanyabiashara 250 kati ya 300 wamepata mafunzo ya namna bora ya kuendesha biashara endelevu na shindani ambapo Wilaya ya Magharibi A (170) na Wilaya ya Chakechake (80). 

 vii. Vituo Jumuishi vya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara vimeanzishwa katika Manispaa ya Musoma, Jiji la Mbeya, jiji la Ilala, jiji la Tanga, na Manispaa ya Moshi ili kurahisisha urasimishaji na uendelezaji wa Biashara. 

Aidha, ujenzi wa vituo hivi numuishi vya jurasimishaji na uendelezaji biashara unaendelea katika manispaa za Iringa, Songea na Shinyanga. 

Kwa upande wa Zanzibar kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara kimeanzishwa katika Baraza la Manispaa la Mjini Magharibi.

Taratibu za ujenzi wa vituo vingine zinaendelea huko Wete Pemba na Unguja.

 viii. Ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za urasimishaji ardhi na biashara umefanyika katika Halmashauri nne (4) za Tanzania Baraambazo ni Magu, Serengeti, Singida na Babati na wilaya Sita (6) za Zanzibar ambazo ni Wete, Mjini, Mkoani, Chakechake, na Magharibi A&B. 

Tathmini imeonesha kuwa wastani wa ushiriki wa wanawake katika biashara ni asilimia 54.25 wakati kwa umiliki wa ardhi ni aslimia 31.75. Aidha, tathmini imeonesha taasis za fedha zinaendelea kukopesha wafanyabiashara na wamiliki wa ardhi zilizorasimishwa ambapo jumla ya shilingi Bilion 2.098 zimetolewa kwa wafanyabiashara wa Singida na Babati wakati shilingi Bilion 1.268 zimetolewa kwa wamiliki wa ardhi wa Halmashauri za Wilaya za Magu na Serengeti. 

Vilevile, asilimia 50% ya migogoro ya ardhi imetatuliwa kutokana na urasimishaji wa ardhi katika halmashauri za wilaya zilizofanyiwa tathmini.



jengo la ofisi ya Masjala ya ardhi ya kijiji cha Nshani, Sumbawanga likiwa katika hatua za ukamilishaji. Ujenzi umewezeshwa na MKURABITA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya pamoja na wananchi wa kijiji hicho

Wafayabiashara na waendesha bodaboda  Manispaa ya Moshi wakipata mafunzo na kufungua akaunti zao za biashara.

       

Ujenzi wa kituo Jumuishi unaendelea katika Halmashauri ya Mji wa Tarime

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana