Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Ndugu Jassery Mwamwala wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za Mwenge 2022, leo katika Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.
Chongolo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba.
Chongolo akisalimiana na Spika mstaafu, Anne Makinda
Chongolo akijadiliana jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) na Naibu Waziri TAMISEMI, Dkt Festo Dugange.
Na Mwandishi Wetu, Njombe
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo ameshiriki Hafla ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 mkoani Njombe.
Mgeni rasmi wa Hafla hiyo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango.
Hafla hiyo imefanyika leo Jumamosi tarehe 02 Aprili, 2022 katika uwanja wa CCM Sabasaba Mkoani Njombe.
Ujumbe wa Mbio za Mwenge 2022 ni, "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo; Shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya Taifa."
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Mawaziri, Makatibu wakuu wa Wizara, Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Post a Comment