Featured

    Featured Posts

MAELFU WALA CHAKULA NA KUSAZA KWENYE KARAMU YA SAUTI YA CHANZO HALISI, ILIYOFANYIKA MAKAO MAKUU YA KANISA HALISI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Maelfu ya Waalikwa na Waumini (uzao) wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, jana Jumapili Februari 26, 2023, walikula na kusaza chakula cha Karamu ya Sauti ya Chanzo Halisi (Mungu Baba), kilichoandaliwa na Kanisa hilo, kutekeleza ilivyoandikwa katika Isaya 25:6-8.
 

Karamu hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, ilifanyika sanjari na Ibada iliyoendeshwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi, somo kuu likiwa kupokea maisha ya urojorojo (raha) katika kila jambo na kila kitu.

Hekaheka za za karamu hiyo ziligubikwa na kila kila mtu kula na kunywa soda na huku maonyesho ya kuuza na kununua bidhaa mbalimbali ikiendelea. 

Tafadhali tazama picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa Karamu. Hizo Hapo👇

Baba Halisi  akimuongezea juisi Mama Halisi wakati wa Karamu hiyo.
Mama Halisi akiwa mwenye furaha wakati akishiriki chakula wakati wa Karamu hiyo.  Virojorojo👇



Wahudumiaji wakiwa tayari kuhudumia uzao.
Faida Halisi akimhudumia soda Uzao.
Mtekeleza Sauti akimhudumia mtoto.
Watoto wakiwa kwenye foleni ya chakula. wote walipata chakutosha.
Uzao wakiwa kwenye hekaheka ya kuhudumiwa chakula.
Uzao wakiwa kwenye hekaheka ya kuhuduma.

Moja Halisi akimhudumia soda Uzao.

Kisha Baba Halisi akagawa supu (chakula) kwa baadhi ya Uzao kwa niaba ya Uzao wote.👇





Uzao wakifanya shukurani kabla ya kushiriki (kula) Supu (chakula) alichowagawia Baba Halisi.
Uzao wakishiriki supu ya urojorojo wa Karamu hiyo.
Mtoto wa Uzao akishiriki supu ya urojorojo wa Karamu hiyo kwa kujinafasi.
Mtekeleza Sauti akishiriki supu ya Karamu hiyo.
Uzao wakifurahi wakati wakishiriki kwa pamoja supu.
Watoto wakila chakula cha karamu hiyo.
Watoto wakishiriki katika Karamu hiyo.
Uzao na watoto wake wakishiriki supu katika Karamu hiyo.
uzao wakishiriki supu katika Karamu hiyo.
Watoto wa Uzao wakishiriki supu katika karamu hiyo.
Mtoto wa uzao akifurahia soda aliyokuwa akinywa wakati wa Karamu hiyo.
Uzao wakishiriki supu wakati wa Karamu hiyo.
Uzao wakishiriki supu wakati wa Karamu.

Mtoto akishiriki Supu kwa utulivu huku soda ya kushushia ikiwa pembeni wakati wa Karamu hiyo.   

Uzalishaji ukiendelea sanjari na Karamu hiyo👇

Uzao akisubiri watenja wa kuweka na kutoa fedha kwenye miamala ya simu za mkononi kwenye Karamu hiyo..
Uzao akisubiri wateja wa nguo za kisasa kwenye Karamu hiyo.
Uzao akiwa na Kuku aliokuwa akiuza mmoja kwa sh. 20,000 na 25,000, kwenye Karamu hiyo.

Uzao akisubiri wateja wa matunda mbalimbali aliyokuwa akiuza kwenye Karamu hiyo.

Baada ya kuhakikisha kila mmoja amekula na kunywa akaendelea kukamilisha Ibada.👇

"Leo naona mmefurahi kupitiliza, maana sasa baada ya kupata urojorojo wa hapa nyumbani kwetu, kila mmoja ataenda kupata urojorojo nyumbani, kila kitu kitakuwa ni urojorojo (raha) tu", akasema Baba Halisi.
"Sasa ni zamu ya kutoa matunda (sadaka), karibuni", akasema Baba Halisi.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Uzao akamsaidia mtoto kutoa matunda Sadaka.
Kisha Baba Halisi akafanya Shukurani ya kuipeleka Ibada kwa kila mtu na mataifa yote👇


Uzao wakipokea shukurani iliyotolewa na Baba Halisi kupeleka Ibada hiyo kwenda kwa watu na mataifa yote.
Uzao wakipokea shukurani iliyotolewa na Baba Halisi kupeleka Ibada hiyo kwenda kwa watu na mataifa yote.
Baba Halisi akabariki kwa kunyuniza damu safi nyeupe (maji) kuzunguka Altare.
Kisha Baba Halisi akamzawadia mtoto mchanga wa Uzao ambaye alifika na mtoto huyo kwenye Ibada. Kisha Wazalishaji (wenye biashara) walifika kwenye Ibada hiyo wakaitwa na kujipanga mbele ya Baba Halisi👇
Wazalishaji (Wafanyabiashara) wakiwa wamejiapnaga mbele ya Baba Halisi.
Baba Halisi akasema na Wazalishaji hao, lakini kabla hajaendelea nao, akamwita Uzao mmoja na kumtia maji ya baraka.👇
Baba Halisi akimnwesha damu safi nyeupe (Maji) uzao aliyemuita kwa sababu maalum.
Kisha Baba Halisi akawanyunyizia maji ya baraka Wazalishaji hao kuwabariki.
Baba Halisi akaendelea kuwabariki Wazalishaji hao.
Baba Halisi akiendelea kuwabariki wazalishaji hao.
Baada ya kuwabariki Baba Halisi akaelekea kwenye eneo lake la kuendeshea Ibada.
Halafu akawabariki tena Wazalishaji hao.
Kisha Baba Halisi akawaaga uzao wote kabla ya kuondoka altareni mwishoni mwa Ibada.
Baba Halisi akisindikizwa na Mnara Mmoja Halisi (katikati) wakati akiondoka mwishoni mwa Ibada.
Mama Halisi pia akafuatia kuondoka baada ya Ibada.
Wapishi wakisafisha vyombo baada ya Sherehe hiyo ya Karamu kumalizika, huku maelfu ya watu wakiwa wamekula na kusaza.  Picha ya Mwisho👇
Mwanamuziki wa Bendi ya nyimbo za kumuinua Chanzo Halisi ya Kanisa Halisi la Mungu Baba King Maluu, akiperuzi gazeti la Uhuru, wakati amepumzika baada ya kumaliza kula chakula cha urojorojo wakati wa Karamu hiyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana