Featured

    Featured Posts

CHONGOLO ASIMIKWA KUWA KIONGOZI WA WAMASAI KONGWA ATOA NENO...


Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesimikwa kuwa kiongozi wa wamasai wakati wa mkutano wa wazi uliofanyika katika Kijiji cha Songambele wilayani Kongwa, Juni 17, 2023.  Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kongwa na kiongozi wa  jamii ya Masai, Mussa Abdi aliyemsimika uongozi huo.

Chongolo akihutubia wananchi na kuwaeleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kwamba ahadi zote zilizomo kwenye Ilani ya CCM kuhusu Jimbo la Kongwa ziatatekelezwa.

Amewaambia kuwa Rais Samia jana Juni 16, 2023, amesaini mikataba ya ujenzi wa  barabara zenye urefu zaidi Km 2000 zitakazojengwa nchini kwa thamani ya zaidi ya sh. trilioni  3 ikiwemo barabara ya Km. 63 inayopita Kongwa hadi Arusha.
Katibu wa NEC  Itikadi na Uenezi wa CCM, Neema Mjema akivishwa golole la kimasai wakati wa mkutano huo.

 Akihutubia wakati wa mkutano huo, Mjema amewataka wananchi kuwapeleka shule watoto wa kike ili baadaye waj.e kuwa watalaam wa nyanja mbalimbali watakaowasaidia wao na Taifa kwa ujumla badala ya kuwatafutia kazi za majumbani


Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu akihutubia katika kutano huo na kuwataka wananchi kujenga ushirikiano na viongozi wa ngazi zote ili kurahisisha utendeji wa kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa ujumla.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana