Featured

    Featured Posts

CHONGOLO: HAKIKISHENI IFIKAPO AGOSTI MNAKAMILISHA MIRADI YA KILIMO KWA VIJANA

 KATIBU Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ametoa maelekezo kwa Wizara ya Kilimo kuhakikisha wanakamilisha miradi ya kilimo kwa Vijana ifikapo Agosti mwaka huu huku akitaka watalaamu kujenga utamaduni wa kukaa kwenye miradi hadi inapokamilika.


Akizungumza leo Juni 17, 2023 akiwa katika ziara yake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, amesema Wizara ya Kilimo inapaswa kukamilisha mradi huo Agosti mwaka huu ili shughuli za kilimo kwa vijana ziweze kuendelea.


Chongolo amesema miradi hiyo inatakiwa ikamilike haraka ili matokeo yaliyo kusudiwa yaanze kuonekana hususan kwa kundi kusudiwa la vijana.


Wakati huo huo Chongolo akiwa katika mradi wa Bwawa la Msagali lililopo kwenye Kata ya Ng'ambi ametumia nafasi hiyo kuwaambia wataalamu kukaa kwenye miradi hadi ikamilike ili inapojitokeza changamoto yoyote wakati wa utekelezaji wa mradi iwe rahisi kitafuta ufumbuzi.


Katibu Mkuu wa CCM Chongolo amemaliza ziara yake wilayani mpwapwa na kuelekea wilaya ya Kongwa kuendelea na ziara yake ya siku nane mkoa wa Dodoma akiwa ameambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu.





author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana