Featured

    Featured Posts

JUMUIYA KUU YA WABAPTIST TANZANIA YAMPONGEZA RAIS SAMIA


Na Lydia Lugakila,

Mwanza


Jumuiya kuu ya Wabaptist  Tanzania  imemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu mingi ikiwemo shule za msingi na sekondari na vituo vya Afya katika maeneo mengi hapa nchini.


Pongeza hizo zimetolewa na Mchungaji Barnaba Michael Ngusa ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania kwa niaba ya Jumuiya hiyo kupitia ibada ya kumsimika Mchungaji Peter Deus Mabawa iliyofanyika Januari 21,2024 katika kabisa la Baptist Nyamanoro Mkoani Mwanza.


Mchungaji Barnaba alisema Rais Samia amewapambania Watanzania na kuwajali katika sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na kujenga na kuboresha miundombinu mingi akiwa halali kwa ajili ya Nchi yake ambapo aliwaomba Watanzania na waumini wa madhehebu mbali mbali hapa Nchini kuzidi kumuombea kiongozi huyo.


Aidha katika hatua nyingine mchungaji Michael alimpongeza Rais Samia,Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa jitahada zao za  kuwarejeshea ardhi Wananchi waliodhurumiwa huku pia akimpongeza  Waziri wa Ardhi Jery Silaa kwa kusimamia vizuri zoezi wa urejeshwaji wa ardhi katika mikoa mbalimbali ikiwemo  Mwanza katika wilaya ya Ilemela ambapo tayari Wananchi wamerejeshewa ardhi zao. 


"Tunamshukuru Mungu na Viongozi wetu imeundwa kamati inayoshughulikia urejeshwaji wa ardhi kwa Wananchi ambapo Pia nako Mkoani Dodoma Wananchi wengi wamerejeshewa ardhi na kupewa hati za umiliki wa Ardhi katika kanisa la Moravian" alisema mchungaji huyo.


Aidha kupitia ibada hiyo  mtumishi huyo wa Mungu aliiomba Serikali kuboreshe baadhi ya miundombinu inayoonekana kusua sua katika baadhi ya maeneo ikiwemo umeme na maji huku akiomba pia zoezi la kurejesha na kutoa hati za umiliki wa ardhi liendelee Nchi nzima ili Wananchi waweze kupata mahali pa kujenga nyumba zao, kupata chakula kutokana na mashamba yao.


Mchungaji Michael alitumia nafasi hiyo kuwaasa waumini wa kanisa hilo kuishi kwa misingi na miongozo ya neno la Mungu na kuachana na mienendo isiyofaa katika kazi ya Mungu.


Alisema kuwa Kanisa hilo litawashughulikia baadhi ya  watu walio nje ya kanisa wenye nia ya kuvuruga kanisa pia kuchonganisha Kanisa hilo na Serikali na jamii na kuleta migogoro katika kazi ya Mungu.


Akiwaongoza waumini hao kupitia neno la Mungu alisema kuwai Viongozi wa kanisa hilo wanapaswa kuwaongoza waumini kwa kutumia neno la Mungu, na kuwa ni vyema waumini waishi kulingana na mafundisho ya kweli ya neno la Mungu na si kuenenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu.

 

"Wakristo ni barua ya Kristo yenya sifa njema iliyotumwa ulimwenguni, ili ulimwengu uisome hivyo watu waache matendo maovu watende mema alisema" mchungaji Barnaba.


Mtumishi huyo aliongeza kuwa Kanisa linatakiwa liwasaidie baadhi ya watu walioingia Kanisani na kutengeneza migogoro na kuwachonganisha viongozi wa Kanisa na waumini ili waichukie serikali inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akiiomba Serikali kuwashughulikia baadhi ya waumini au watu wanaoleta migogoro na migongano ikiwemo ya kimaslahi na kimadaraka katika nyumba za ibada.


Ikumbukwe kuwa Ibada ya kumsimika Mchungaji Deus Peter Mabawa ilifanyika ikiwa ni kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na  Mchungaji Isaac Madeleke aliyefariki miaka miwili iliyopita.

DK. NCHIMBI AMPONGEZA CHONGOLO KWA KUKIIMARISHA CHAMA


 Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya CCM amemshukuru na kumpongeza mtangulizi wake Komredi Daniel Chongolo kwa kazi kubwa aliyoifanyia CCM tofauti na alivyoikuta.


Pongezi hizo amezitoa alipokuwa akihutubia wakati wa mapokezi yaliyofanyika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma Januari 22, 2024.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

KOMREDI CHONGOLO AMKABIDHI OFISI DK. NCHIMBI

 


 Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Daniel Godfrey Chongolo akimkabidhi nyaraka mbalimbali Katibu Mkuu mpya wa CCM Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya nafasi hiyo katika shughuli maalum iliyofanyika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma Januari 22, 2024.

RAIS DK. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA HUU WA CDF NA MAKAMANDA, LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Jacob John Mkunda, wakati wa mkutano wa CDF na Makamanda kwa mwaka 2023 ambao ulifanyika Lugalo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Januari, 2024.
 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Maafisa Majenerali mbalimbali wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati akifungua mkutano wa CDF na Makamanda uliofanyika Lugalo Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Maafisa Majenerali mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Maafisa Majenerali mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa kwenye Mkutano huo.Amiri Jeshi Mkuu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Wanawake wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), baada ya kufungua Mkutano huo.

DKT NCHIMBI ALAKIWA KIMILA DODOMA

 

Wazee wa kimila wakimvisha mgolole ikiwa ni ishara ya kumsimika Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapimduzi (CCM), DKT. Emmanuel Nchimbi kuwa Chifu wa kabila la wagogo katika hafla iliyofanyika wakati wa mapokezi yake katika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma Januari 23, 2024.
Akikabidhiwa ngao
Akikabidhiwa mkuki


 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203

DKT NCHIMBI ATINGA MAKAO MAKUU YA CCM DODOMA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Emmanuel Nchimbi akiwasili Makao Makuu ya chama hicho wakati wa mapokezi jijini Dodoma Januari 23, 2025.
Dkt . Nchimbi akivishwa skafu na vijana wa UVCCM
Dkt. Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Dodoma, Neema Majule.
Msafara wa Dkt. Nchimbi ukitokea Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwenda Makao Makuu ya CCM.
Dkt. Nchimbi akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa.

Dkt. Nchimbi akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Anamring Macha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Mary Chatanda akiwa miongoni mwa viongozi walioshiriki mapokezi ya Dkt Nchimi.
Sehemu ya wanachama na wafuasi wa CCM



IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203
 

BALOZI DK. NCHIMBI ALIVYODHIHIRISHA KUWA MWANADIPLOMASIA ALIYEIVA, AWAPA 'AKILI' CHADEMA WASITUMIE MIGUU KUJENGA HOJA, WAJITOFAUTISHE NA MASHINDANO YA UREMBO AMBAYO NYENZO KUU NI UHODARI WA KUTEMBEA

Na Bashir Nkoromo, CCM Official CCM Blog, Dar es Salaam
Akizungumza katika mkutano wa mapokezi yake yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana, Januari 20, 2023, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi aliweza kudhihirisha kuwa siyo mwanasiasa nguli tu bali pia ni Mwanadipromasia aliyeiva.

Miongoni mwa yaliyoonesha kuiva Kidiplomasia na kisiasa ni namna alivyowapa 'madongo makavu' kistaarabu baadhi ya vyama vya upinzani hususan Chadema wanaoelekea kuwepa mazungumzo ili kujenga hoja zao, badala yake kukimbilia kufanya maadamano kutibua michakato mizuri ya kitaifa inayoendele nchini.

Pia ni namna alivyofikisha ujumbe mzito kwa wana wa CCM katika kukijenga na kukiimarisha Chama na namna ya CCM kuzoa ushindi Mkubwa katika Uchagzi wa serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Katika mkutano huo, baada ya kukaribishwa jukwaani na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtevu Balozi Dk. Chimbi kwanza aliwashukuru viongozi na wananchi hususan wana CCM, kwa mapokezi bora aliyopata licha ya hali ya hewa ya mkoa huo kutingwa na hekaheka ya mvua iliyoharibu hadi baadhi ya madaja na barabara katika maeneo kadhaa.

Kisha akamualika Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na Afisa Mwandamizi wa Makao makuu ya CCM Frank Uhahula ili kusalinia hadhara kabla ya kuendelea na hotuba yake. RC Chalamila alimualika kwa ajili ya nafasi yake, lakini Uhahula alimualika kwa sababu maalum.

Japokuwa la 'vidonge' kwa vyama vya siasa aliliachilia karibu na mwisho wa hotuba yake, lakini naomba ndiyo nitangulize kwa kuwa lilionyesha kuwakuna wengi waliohudhuria mkutano huo na kusabisha kushangilia mno, bila shaka kutokana na umuhimu wa ujumbe na namna Balozi Dk. Nchimbi alivyokuwa akiufikisha.

VYAMA VYA SIASA TUENDELEE KUSHIRIKIANA ILI KUTIMIZA WAJIBU WA URAIA WA NCHI YETU
"Kuhusu vyama vya Siasa, tunavyo vyama vya siasa ambavyo vinashiriki katika siasa za nchi yetu, nitumie nafasi hii kwanza kuviomba tuendelee kushirikiana kwa sababu wote tunatimiza wajibu wa uraia wa nchi yetu.  

Na milango ya ofisi ya Katibu Kkuu itakuwa wazi kwa vyama vya siasa vingine na tupo tayari kushirikiana tukijua kwamba sisi wote ni wadau wa maelndeleo ya nchi yetu, wote tuna nia ya kueleta maendeleo ya nchi yetu.

Lakini hiyo haitamaanisha kwamba kasi ya kutafuta ushindi mkubwa zaidi itapungua, tutaendelea kushirikiana nao, kupendana nao lakini tutaendelea kutafuta viti vingi zaidi Bungeni na Serikali za mitaa, lakini pia ushindi wa kishindo kwenye Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar", akasema Balozo Dk. Nchimbi, kisha akaongeza;

"Yapo mazungumzo mbalimbali yanayoendelea, Chama Cha Mapinduzi, kimedhamiria kuendelea na mazungumzo katika kuboresha sheria mbalimbali, tumeshashirikisha wadau wa aina mablimabli katika mazungumzo haya, tutaendelea kuwashirikisha, kwa sababu dhamira ya Rais wetu ni kuona kwamba kila Mtanzania anashirikishwa katika kuamua mambo ya msingi ya nchi yetu.

Naomba wadau wote wa maendeleo vikiwemo vyama vya siasa vitambue kwamba dhnara ya mazungmzo lazima iakisi pande zote, iakisi ndani ya CCM, vyama na wadau.

KUKWEPA MAZUNGUMZO SIYO UJASIRI, NI DALILI YA WOGA.
Kususia mazungumzo, kutaka kukwepa mazungumzo siyo ujasiri, kukimbia mazungumzo na kutaka kukwepa mazungumzo ni dalili ya woga, kutaka kukimbilia maandamano ni dalili ya woga, hoja zinajengwa kwa mdomo hazijengwi kwa miguu.  Maana ukitaka kujenga hoja kwa maandamano maana yake unataka kujenga hoja kwa miguu badala ya kujenga hoja kwa ubongo.

Kwa hiyo wakiandamana tutawatazama, lakini wajue hatutawapima kwa kasi za miguu yao, tutawapima kwa hoja zao, maana wasije wakadhani, tukiwatizama wakitembea wakati wanaadamana tunasema eti kwa mwendo ule huyu ana hoja.

JITOTOFAUTISHENI NA MASHINDANO YA UREMBO, AMBAYO NYENZO KUBWA NI KUTEMBEA, JENGENI HOJA KWA UBONGO SIYO KWA MIGUU
Sasa vyama vya siasa lazima vijitofautshe na mashindano ya urembo, maana kwenye mashindano ya urembo hupimwa katika mwendo unatembeaje. Kuna staili za kutembea, kuna 'cut walks' mwendo wa paka , mwendo wa panya, sijui nini.. 'you know'", akasema Balozo Dk. Nchimbi, halafu akamalizia akisema;

Sasa lazima wapinzani wajitofautishe na kuwa taswira ya mashindano ya urembo, tujenge hoja tusikimbilie maandamano, lakini wakitaka kuandamana tunawatakia heri. Na wasihi wa CCM na Watanzania kwa jumla, mtakapowaona wanaandamana kwa ajili ya kushidwa majadiliano basi muwaangalie miguu yao, mtambue wametumia miguu kufikiri.

UJUMBE KWA WANA CCM
"Nianze kuwashukuru ndugu wanachama chini ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa kwa mapokezi yenu ya kipekee, naomba nikiri kwamba nilipopewa taarifa ya hali ya mvua jinsi madaraja yalivyokatika maeneo mbalimbali nikasema naomba tuahirishe tu huo mkutano, lakini Mwenyekiti akasema hapana, tusiahirishe, hao hao watakaokuwepo ndiyo tuzungumze nao.

Waliponiambia njoo hao hao tuzungumze  nao nilifikiri nitakuta watu 50! lakini nimestuka kweli, mahudhurio haya pamoja na mvua na kukatika madajara. Kwa hiyo kwa dhati kabisa nawahshukuruni sana kwa mapenzi yenu kwa Chama chetu, Mwenyekiti na timu yako nawashukuru sana kwa maandalizi ya kipekee. na wadau wote mlioshirikiana kufanikisha mapokezi haya nawashukuruni sana sana", akasema Balozo Dk. Nchimbi.

"La pili niendelee kumshukuru Rais wetu, Mwenyekiti wa Chama tetu Dk. Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa aliyonipa ya kunipendekeza kuwa Katibu Mkuu wa Chama chetu na hatimaye kuteuliwa na vikao vya Chama. Narudia kumhakikishia kuwa mimi na wasaidizi wangu na timu yangu ya sekretarieti tutafanya kila linalowezekana tusiangushe imani aliyotupa.

La tatu naomba niwafikishie salam za Mwenyekiti, nimemtaaifu kuwa leo ninashughuli na wana Dar es Salaam, ameniambia niwaambie kuwa anawapenda anawashukuru kwa kazi mnayofanya ya Chama na yupo tayari kuendelea kushirikiana nanyi kujenga Chama chetu", akasema tena Balozi Dk. Nchimbi.

Katika kuhimisha Salam kutoka kwa Mwenyekiti Rais Dk Samia, akasema; "..Kuna maneno nimeyasikia hapa akisema Mwenyekiti..., alisema Samiaaaa...,", akasema Balozo Dk. Nchimbi mkutano ukalipuka.. "Mitano tenaaaa, Kazi Iendelee". Kisha Balozo Dk. Nchimbi akahitisha kwa kibwagizo "Mambo ya msingi hayataki aibu".

Kisha Balozi Dk. Nchimbi akaendelea kuhutubia akisema, "La nne namshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kwa ahadi aliyoitoa ya kushughulikia mafuriko yaliyotokea maeneo mbalimbali ya mkoa wake leo. nilikusudia kumuomba atusaidie kufanyakazi kwa haraka ahakikishe mkoa wanafanya kazi kwa haraka kupambana na changamoto zilizotokea lakini kiongozi makini hakusubiri maelekezo, yeye mwenyewe ametangulia kusema tutafanya moja mbili tatu.. nawashuku, mkatekeleze mliyotuahidi".
 

KATIKA USIMAMIZI ILANI YA CCM, KAZI KUBWA IMEFANYIKA CHINI YA RAIS DK. SAMIA
"Nitumie nafasi hii kuipongeza sana serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, na Serikali zetu mbili na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla wake, kazi ambazo zimefanyika kwa miaka hii mitatu siyo ya kitoto, Chama chetu kimeweza kuzisimamia serikali zake chini ya Mwenyekiti wa Chama Dk. Samia Suluhu Hassani, kuhakikisha kwamba kazi kubwa inafanyika.

Baadaye tutakuwa na kazi ya kueleza kwa kina mambo ambayo Serikali za Chama Cha Mapinduzi zimefanya katika nchi yetu, mambo ambayo kwa kweli ni ya kujivunia sana,  Wana CCM lazima watembee kifua mbele wakijiamaini wakionyesha kazi zilizofanywa na Chama chetu, kazi zilizofanywa na Serikali zetu,  Msionee aibu mafanikio tuliyoyapata, kila nafasi mtakayopata ya kuelezea mafanikio ya serikali za CCM msione aibu kuyaeleza", akasema Balozi Dk. Nchimbi.


UHAKIKA CCM KUSHINDA MITAA, UCHAGUZI MKUU
"Na mimi nina uhakika kama alivyosema Mwenyekiti tukizieleza kwa umakini kazi zetu tulizozifanya, tukiwafanya watu wetu waelewe kazi zilizofanyika, bahati nzuri zinaonekana, kwa kuwa tumeshazifanya, hakuna sababu hata moja ya Chama chetu kutopata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Kwa hiyo wakati tukijiandaa kupata ushindi mkubwa, lakini tuzidi kuwaelekeza kwa kuwaleza wananchi wetu na kuwaonyesha kazi tulizofanya, na tuifanye kazi hii kwa nguvu usiku na mchana, ninaamini kabisa kabisa, tukifanya kazi hii ya kuwakumbusha wenzetu kazi zilizotekelezwa na Serikali za CCM, basi Watazania hawatakuwa na sababu hata moja ya kutoendelea kuaiamini na kutoendelea kuichagua CCM, na kwa maana hiyo Chama chetu kitaendele kushinda na kushinda.

TUNAPOENDELEA KUSHINDA, HATUPASWI TUWE NA KIBURI.
"Lakini kadiri tunapoendelea kushinda hatupaswi kuwa na kiburi lazima tujikumbushe kuwa kwamba Chama Cha Mapinduzi ni  Chama cha Wananchi, ni Chama cha wanyonge. Wana CCM ni lazima wajue kwamba wanabeba dhima kubwa ya kuhakikisha kwamba wanaenzi heshima yao kwa Watanzania kwa Chama chao kwa kufanya kazi kwa juhudi.  

Kwa hiyo nasisitiza sana namna ambavyo Chama chetu kinaendelea kuzisimamia vema serikali zake kwa umakini zaidi kuona kwamba zinzendelea kutekeleza ilani ya Chama katika maeneo machache yaliyobaki ili tupate ushindi wa kishindo, na nina hakika ushindi tutakaopata kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani utakuwa mkubwa sana sana.

CHAMA KISIKWEPE WAJIBU WAKE WA KUISIMAMIA SERIKALI, VIONGOZI WA SERIKALI WASITUKANWE.
"Chama chetu kisikwepe wajibu wake wa kuzisimamia serikali, ni wajibu wa kikatiba ni wajibu wa kikanuni, tunapoomba kura kwa wananchi tunaenda na Ilani ya Uchaguzi ya Chama tukichaguliwa maana yake wananchi na CCM ndiyo wenye mkataba, na mtekelezaji wa ule mkataba ni serikali za CCM kwa hiyo CCM haipaswi kuona haya kuzisimamia serikali.

Lakini tuzisisimaime bila kuwa na kiburi tuzisimamie kwa weledi, hatuwezi kuzisimamia serikali kwa kutukanatukana watu, ohh hapa kwa nini matofali saba hayapo.., mshenzi sana wewe,  hapana, mshenzi haipo katika ilani ya CCM, lazima tuwaheshimu watumishi wa serikali, tuongoze kwa weledi.

Kila mtu anajua Chama Cha Mapinduzi ndicho kinachotawala hatuhitaji kubeba rungu kubwa kuonyesha kuwa CCM ndicho kinachotawala na tunatawala kwa niaba ya wananchi, kwa hiyo viongozi wa Chama msione haya kusimamia, lakini msimamie kwa weledi, tuhakikishe viongozi wetu wa serikali wanafanya kazi vizuri wakijua kwamba chama chao kinawasimamia lakini pia kinawapenda na kuwaheshimu, na  kwa kufanya hivyo ni wazi kwamba tutaendelea kupata mafanikio makubwa sasa na siku za usoni", akasema Balozi Dk. Nchimbi.

CHAMA CHINI YA RAIS DK. SAMIA KITAENDELEA KUTIMIZA WAJIBU WAKE, TUNACHOFANYA TUTAONGEZA TU KASI.
Balozi Dk. Nchimbi akiendele kuzungumza bila mbwembwe akasema; "Na kwa hiyo nimesimama hapa kuwahakikishieni kwamba Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wetu, Rais Samia kitaendelea kutimiza wajibu wake wa kuzisimamia serikali, tunachofanya tutaongeza tu kasi, kwamba tulikuwa gia namba 3 mwendo umekolea tunaenda namba 4 sababu hatuwezi kukimbia na gia moja tu kwa mwendo wa kilometa 20, kuna mda lazima ubadili gia, na nchi yetu bado masikini bado tunatumia gia za kizamani hatuwezi kutumia 'automatic' katika nchi ambayo bado inakua,

Kwa hiyo sasa ni wakati wa kuongeza kasi zaidi, wana CCM wote wajiandae kuongeza kasi zaidi kutafuta ushindi wa chama, lakini pia kutafuta utekelezaji wa ilani uliotukuka wa Chama Cha Mapinduzi.

RC CHALAMILA: DK. NCHIMBI ANA MOYO WA KUTOKUWA MNAFIKI KATIKA UTUMISHI NA HILI NDIYO SILAHA YAKE.
Awali, kabla Balozi Dk. Nchimbi kuanza hotuba yake alimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila kusalimia umma, RC Chalamila akasimama jukwaani, akatoa salam ya Chama, kisha akasema; "wote tupunge mikono". Wakapunga halafu akaendelea; "Ndugu Katibu Mkuu Dar es Salaam ni salama tunakukaribisha.

Dk. Nchimbi mara nyingi ana moyo wa kutokuwa mnafiki katika utumishi wa kazi zake, na hili ndiyo silaha yake kubwa sana katika utumishi wa kazi serikali na ambalo pia ataenda nalo katika utumishi wa Chama. Mimi naomba nikuthibitishie kuwa sisi viongozi wa serikali, katika mkoa huu tumejipanga kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi vizuri ili Chama kisipate taabu kwenye chaguzi zake.
 
Na tutafanya hivyo, lakini zaidi pia Mheshimiwa Katibu Mkuu tuelekezeni muda wowote, na hapa nikitoka tunakwenda mahali ambako maji yamefanya uharibifu wa barabara. Nakuhakikisishia Mheshimiwa Katibu Mkuu kesho barabara zitapitika. Kidumu Chama Cha Mapinduzi." akahitimisha RC Chalamika na Kisha Katibu Mkuu akamsifu akisema, "Sauti yake (RC Chalamila) ina mirindimo ya CCM".

UHAHULA: TUMEPATA KATIBU MKUU, SIYO ALIYEPITIA UVCCM BALI ALIYETOKANA NA UVCCM. CCM CHINI YA MIKONO YA DK. NCHIMBI IPO SALAMA.
 Baada ya RC Chalamika Balozi Dk. Nchimbi akamualika Afisa Mwandamizi wa Makao Makuu ya CCM Frank Uhahula, akisema;  "Lakini pia nitampa nafasi mtu mwingine mmoja. Huyu mtu mmoja nilipogombea mara ya kwanza Uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Taifa ndiye aliyenivuruga kuliko wote. Hatari sana mtu huyo. Mtu huyo anaitwa Frank Uhahula. Frank njoo usalimie".

Uhahula akasimama jukwaani akasema; "...Ndugu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Balozi Dk. Emanuel John Alfonso Nchimbi, nafahamu hadhara hii si yangu, lakini kwa unyenyekevu mkubwa na heshima kubwa umeamua kunipa nafasi, umenipa nafasi ya kusalimia katika mkutano huu, naomba nikushukuru sana.

Langu mimi ni moja tu. Tumepata Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Katibu Mkuu siyo aliyepitia Umoja wa Vijana, bali ni katibu Mkuu anayetokana umoja wa Vijana. Umoja wa Vijana kama chombo cha Chama umepewa dhamana ya kuwa tanuru la kuandaa na kupika si tu viongozi, bali viongozi wa juu wa chama chetu.

Hakuna mashaka hata kidogo kwamba chama hiki chini ya mtendaji mkuu wa Balozi Dk. Nchimbi kipo salama. Anakifahamu Chama Cha Mapinduzi  kushoto, kulia, mblele, nyuma na katikati na anaifahamu serikali vizuri.

Balozi Dk. Nchimbi anajua siasa za kugombea maana kuna viongozi wanachanguliwa lakini sasa kugombea hawajui, kwa hiyo ana 'experience' hiyo. Mimi naamini kabisa tupo salama.  Sisi wote, Viongozi wa Chama, Viongozi wa serikali, Wanachama wa CCM na Watanzania wote tuungane naye ili kupitia yeye tumsaidie Rais wetu ili tuwe na ushindi mkubwa mwaka huu na mwakani".

DK. NCHIMBI MOYO NINAOUTAKA NDANI YA WANA CCM, NI KUJUA UCHAGUZI SIYO UGOMVI
"Nimemsimamisha Frank kwa sababu miaka 25 imepita tangu nilipogombea naye,  lakini moyo ninaoutaka ndani ya wana CCM ni kujua kwamba uchaguzi siyo ugomvi. Pamoja na kupita miaka 25 bado katika siasa za UVCCM ndiye ninayemheshimu zaidi kwa sababu shughuli haikuwa ndogo, maana tulipiga kura raundi ya kwanza hakuna aliyevuka nusu, mimi na yeye tukarudia raundi ya pili, na bado tupo marafiki mpaka sasa, kuna wengine wenezetu wakigombea wananuniana mpaka kiyama", akasema Balozo Nchimbi baada ya salam za Uhahula.

SERA YANGU KATIKA MIAKA YOTE YA UTUMISHI WA UMMA NA CHAMA NI  MANENO KIDOGO KAZI ZAIDI
Akihitimisha houba yake Balozi Dk. Nchimbi alieleza msimamo wa utendaji wake akiweka wazi kwamba ni wa maneno kidogo kazi zaidi.

"Sera yangu kwa miaka yote ambayo nimekuwa katika utumishi wa umma na Chama chetu ni maneno kidogo kazi zaidi, ndiyo maana wananchi wa Songea Mjini (alikokuwa Mbunge), ukienda kuwaambia maneno kidogo watakuambia kazi zaidi, kwa sababu kwa miaka kumi ndiyo ilikuwa sera yetu ya kufanyia kazi na CCM. Sekretarieti ninayoiongoza katika miaka hii nitakayokuwepo tutafanya kazi zaidi ili tupate tija zaidi, tija itapatikana zaidi kwa kufanya kazi zaidi.

LAZIMA TUENDELEE KUANDAA CHIPUKIZI KUWA VIONGOZI WA NCHI YETU, WANAOFIKIRI CHIPUKIZI HAINA MAANA WANA NIA MBAYA NA CCM.
"Chipukizi wamenikumbusha mbali, tukiwa wadogo, Uhahula ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Chipukizi wa taifa, kuna baadhi ya watu wanafikiri Chipukizi haina maana kusema kweli wanaofikiri hivyo wana nia mbaya na Chama chetu, lazima tuendelee kuandaa Chipukizi  tuwaandae kuwa viongozi wa nchi yetu.

Kiongozi kama hujaandaliwa kuna wakati utapata taabu, utakimbizwa huku ukakimbia, unanweza ukakimbia huku, unaweza kuwa mtu unayeyumbayumba bila utaratibu, tulisionee haya jambo hili, nimeona Chipukizi mwili ukasisimka", akasema Balozi Dk. Nchimbi akiwashukuru Chipukizi waliomvisha skafu wakati akiwasili eneo la tukio.

DAR SIYO MGENI, NAZIJUA CHOCHORO ZOTE ZA KUOMBEA KURA.
"Nawashukuru kwa mapokezi haya, mimi siyo mgeni hapa Dar es Salaam, nilikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu wilaya ya Ilala nikiwa na umri wa miaka 21, chochoro zote za kuombea kura nazijua, kwa hiyo tutashirikiana.  Nawapenda, nitawatumikia, nitahakikisha Chama chetu na Serikali zetu zinafanya kazi kwa nguvu zote. Asanteni", Balozi Dk. Nchimbi akahitimisha hotuba yake mwanana, papo hapo ikasindikizwa na nderemo, hoi, hoi za kumshangilia.

Balozi Dk. Nchimbi jina lake lilipendekezwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia na baadaye kupishwa kwa kauli moja na vikao vya Chama vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, vilivyofanyika mjini Zanzibar, hivi majuzi, akichukua nafasi iliyoachwa na Daniel Chongolo ambaye alijiuzulu.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa vitendea kazi na Mwakilishi wa Baraza la Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Yahya Ngoma, wakati wa mkutano wa mapokezi yake, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana, Januari 20, 2024. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Abbas Mtemvu na kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu. Mtiririko wa picha tangu mwanzo hadi mwisho wa tukio👇

Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) ikitumbuiza kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi kuwasili.
Mkurugenzi wa TOT Khadija Kopa akiimba wimbo wa hamasa wakati Katibu Mkuu wa CCM Balozo Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili Uwanjani.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwa gari lake Uwanjani.
Wana CCM wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akiwasili Uwanjani.
"Mheshimiwa, pita huku", Afisa Itifaki kutoka Idara ya Siasa na Uhuano wa Kimataifa (SUKI) Makao Makuu ya CCM akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Nchimbi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Anamringi Macha. Katikati ni Abbas Mtemvu akifurahia.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Nchimbi akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda.
"Kwa hiyo sasa tunasimama hapa, au?" Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akimuuliza Mwenyekiti Abbas Mtemvu. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Adamu Ngalawa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akiwa na baadhi ya Wakuu wa Wilaya za mkoani humo.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akisubiri kuvishwa skafu.
Chipukizi hodari wa CCM akimpa saluti Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi kisha kumkaribisha na kuwa tayari kuvishwa skafu.
Chipukizi wa CCM akimvisha skafu Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akitembea kikakamavu kwenda jukwaa kuu, huku akiongozana na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM. Kulia ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Anamringi Macha.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akipita katika umati wa wana CCM wakati akienda meza kuu.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akienda meza kuu.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akiwa tayari meza kuu huku akishangiliwa na wliohudhuria mkutano huo. Kulia naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Anamringi Macha na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed (Dimwa) na Abbas Mtemvu.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akishiriki kuimba wimbo wa taifa.
Wana CCM wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi na viongozi wa meza kuu wakishangilia baada ya wimbo wa taifa.
Hekaheka zikirindima uwanjani baada ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi kuketi.
Hekaheka zikirindima uwanjani baada ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi kuketi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa vitendea kazi na Mwakilishi wa Baraza la Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Yahya Ngoma, wakati wa mkutano wa mapokezi yake, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana, Januari 20, 2024. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Abbas Mtemvu na kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa vitendea kazi na Mwakilishi wa Baraza la Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Yahya Ngoma, wakati wa mkutano wa mapokezi yake, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana, Januari 20, 2024.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akimshukuru Mwakilishi wa Baraza la Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Yahya Ngoma, baada ya kupokea vitendea kazi.
Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya viongozi na wana CCM wengine wakiwa kwenye mkutano huo.
Wazee wa Baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akitazama kwa shauku kabla ya kuanza kuwahutubia wana CCM waliohudhuria mkutano huo.
"Dk. Nchimbi juu, CCM juuuuu", akisema Afisa Mwandamizi wa Makao Makuu ya CCM Frank Uhahula baada ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi kumkaribisha kusalimia.
"Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia juuuuu", akasema Uhahula.
"Langu mimi ni moja tu. Tumepata Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Katibu Mkuu siyo aliyepitia Umoja wa Vijana, bali ni katibu Mkuu anayetokana umoja wa Vijana. Hakuna mashaka hata kidogo kwamba chama hiki chini ya mtendaji mkuu wa Balozi Dk. Nchimbi kipo salama". akasema Uhahula.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akianza hotuba yake.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akiendelea kuwahutubia wana CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akiendelea kudadavua mambo mbalimbali wakati akihutubia wana CCM. Picha za ziada👇
RC Chalamila akiwa na baadhi ya Maafisa waandamizi wa Makao Makuu ya CCM (kushoto) nje ya Uwanja wa Mnazi Mmoja alipowasili kweneye mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed (Dimwa) akimsalimia kwa upendo Afisa Mwandamizi Mstaafu wa makao Makuu ya CCM Mary Nchimbi wakati akiwasili kwenye mkutano huo.
 
Raia wa Ujerumani wakinunua kofia kwa wauzaji waliokuwa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa mkutano huo.

Imeandaliwa na Bashir Nkoromo, Msimamizi Mkuu Blog ya Taifa ya CCM. Januari 21, 2024.
 

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

JUMUIYA KUU YA WABAPTIST TANZANIA YAMPONGEZA RAIS SAMIA

Na Lydia Lugakila, Mwanza Jumuiya kuu ya Wabaptist  Tanzania  imemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt...

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana